Tuesday, June 3, 2014

ROAD TO BRAZIL: SCOLARI AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUSHINDA KOMBE LA DUNIA ILI KUWAPOZA MASHABIKI WA NCHI HIYO.

KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil amewataka wachezaji wake kushinda taji la Kombe la Dunia kwa ajili ya uenyeji wao wa micuano hiyo. Mabingwa hao mara tano wa michuano hiyo wanatarajiwa kucheza mechi yao ufunguzi pale watakapoikaribisha Croatia Juni 12 jijini Sao Paulo. Wakati homa ya michuano hiyo ikizidi kupanda katika miezi hii ya karibuni, maandalizi ya michuano hiyo kwa Brazil yamekumbwa na maandamano ya mara kwa mara watu wakipinga gharama kubwa zilitumiwa kwa ajili ya maandalizi huku pia kukiwa na changamoto kwa baadhi ya viwanja kushindwa kukamilika kwa wakati. Kutokana na hayo yote Scolari anaamini kunyakuwa taji hilo kutawaunganisha mashabiki wa nchi hiyo kuwa kitu kimoja. Akihojiwa Scolari amesema wakati Brazil inacheza michuano hiyo watu wanategemea kushinda taji hilo, na suala hilo haliwasumbui kwasababu ni jambo la kawaida kwa mashabiki wa soka nchi hiyo pamoja na wachezaji. Scolari aliongeza anajua kuwa kuna matatizo katika maandalizi na watu hawajafurahishwa kutokana na baadhi ya mambo ndio maana anasema ni wajibu kuwafurahisha kwa kuhakikisha taji hilo linabaki katika ardhi yao. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa soka nchini Brazil ni kama dini hivyo ni kawaida kuwa chini ya shinikizo lakini anadhani hilo ni jambo zuri kwa wachezaji kwani hawawezi kusahau malengo yao.


No comments:

Post a Comment