Tuesday, June 3, 2014

ROAD TO BRAZIL: VAN GAAL ASIKITIKA KUWAKOSA KINA BALE NA RAMSEY KATIK MECHI YA KIRAFIKI DHIDI YA WALES.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal amesema amesikitishwa kuwa timu yake itakutana na timu ya taifa ya Wales kesho kwa ajili ya mchezo wa kirafiki bila kuwa na nyota wake Gareth Bale na Aaron Ramsey. Bale mwenye umri wa miaka 24 anayecheza katika klabu ya Real Madrid amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya msuli kwa wiki kadhaa wakati nyota wa Arsenal, Ramsey mwenye umri wa miaka 23 amepumzika. Mechi hiyo ya kirafiki inayotarajiw akupigwa katika Uwanja wa Amsterdam Arena ni sehemu ya maandalizi ya Uholanzi kwa ajili ya Kombe la Dunia. Van Gaal amesema aliiambia bodi kuwa wanatakiwa kusisitiza kuwa Wales wawachezeshe Bale na Ramsey lakini haelewi kumetokea nini, kwani kama ni majeruhi anaweza kuelewa lakini kama ni mapumziko atakuwa hajafurahishwa na hilo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ni vyema kucheza na kikosi bora cha wa Wales ili waweze kupata upinzani lakini bila wachezaji hao anadhani kikosi cha nchi hiyo kitakuwa dhaifu.


No comments:

Post a Comment