MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez amesema hakuna nafasi ya yeye kuikosa michuano ya Kombe la Dunia kiangazi hiki kutokana na majeruhi. Nyota wa klabu ya Liverpool alilazimika kufanyiwa upasuaji mdogo wa goti mwezi uliopita, hivyo kuzusha hofu kuwa ataikosa michuano hiyo itakayofanyika nchini Brazil. Hata hivyo, Suarez amebainisha kuwa haitawezekana kwa yeye kuikosa michuano hiyo kwasababu anajisikia vyema. Suarez amesema hakuna mahali alipojisikia kuwa anaweza kuikosa michuano hiyo kwasababu alikuwa na uhakika anaweza kupona kwa wakati na kuisaidia nchi yake. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa wakati akizungumza na daktari kuhusu upasuaji wake kidogo machozi yamtoke lakini alijikaza mpaka mke wake akamshangaa kwa ujasiri wake lakini hiyo ni kwasababu alijua anaweza kuvuka kikwazo hicho.

No comments:
Post a Comment