Friday, July 11, 2014

ATLETICO YATHIBITISHA KUMCHUKUA MANDZUKIC KUZIBA PENGO LA COSTA.

KLABU ya Atletico Madrid, imethibitisha kumsajili mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Croatia kwa mkataba wa miaka akitokea Bayern Munich ya Ujerumani. Mabingwa hao wa Hispania wamefanya uamuzi wa haraka kumchukua nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 baada ya mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Diego Costa kusiani mkataba wa kuichezea Chelsea msimu ujao. Mandzukic amekuwa kama mchezaji asiyekuwa na namba ya kudumu Bayern kufuatia ujio wa mshambuliaji Robert Lewandowski kutoka kwa mahasimu wao wa Bundesliga Borussia Dortmund. Mkurugenzi wa michezo wa Atletico Jose Luis Perez Caminero ndio aliyethibitisha taarifa hizo katika mtandao wa klabu hiyo na kudai kuwa ujio wa Mandzukic ni muhimu kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa na Costa. Mandzukic ameichezea Bayern kwa misimu miwili na kufunga mabao 33 katika mechi 54 za Bundesliga alizocheza huku akifnga bao la kuongoza la Bayern dhidi ya Dortmund katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2013 ambapo Bayern walishinda mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment