MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amebubujikwa na machozi wakati akielezea majeruhi yaliyomaliza ndoto zake za kucheza michuano ya Kombe la Dunia kuwa yangeweza kumuacha akiwa melmavu. Nyota huyo wa klabu ya Barcelona mwenye umri wa miaka 22, alivunjika mfupa katika uti wake wa mgongo wakati alipopigwa kwa goti na beki wa Colombia Juan Zuniga katika mchez baina ya timu hizo katika hatua ya robo fainali. Akizungumza na waandishi wa habari Neymar amesema mungu alimsaidia kwani kama tukio hilo lingezidi kwa sentimita mbili zaidi angekuwa anatembelea baiskeli ya magurudumu. Zuniga alimuomba radhi Neymar na FIFA wakadai hakuna hatua yoyote ya kinidhamu inayoweza kuchukuliwa kwasbabu tukio hilo lilionwa na mwamuzi Velasco Carballo aliyechezesha mchezo huo. Neymar amesema hamchukii Zuniga kwa tukio hilo na wala hadhani kama alilifanya makusudi lakini kila mtu anayefahamu soka ataona faulo ile haikuwa ya kawaida.

No comments:
Post a Comment