Tuesday, July 15, 2014

FARAH HATIHATI KUSHIRIKI JUMUIYA YA MADOLA.

MWANARIADHA nyota wa Uingereza na bingwa mara mbili wa michuano ya olimpiki na dunia, Mo Farah amezusha hofu ya kutokuwa fiti kushiriki michuano ya Jumuiya Madola. Farah mwenye umri wa miaka 31 alikuwa amepanga kukimbia mbio za mita 5,000 na 10,000 katika michuano hiyo inayotarajiw akufanyika baadae mwezi huu huko jijini Glasgow, Scotland. Lakini alijitoa katika mashindano ya Diamond League yaliyofanyika huko Hampden Park kwasababu ya kuumwa. Akiulizwa kama atakuwa fiti kwa ajili ya michuano ya Jumuiya ya Madola, Farah amesema hana uhakika na hilo ila anategemea atakuwa vizuri pamoja na kwamba amekosa mazoezi kidogo. Farah alipelekwa hospitali nchini Marekani kutokana na maumivu ya tumbo mwanzoni mwa mwezi huu na kufanyiwa vipimo zaidi nchini Uingereza na daktari wake tayari ameshamruhusu kuanza mazoezi lakini haijathibitika kama atakuwa fiti kwa ajili ya michuano hiyo. Michuano ya Jumuiya ya Madola inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumapili ya Julai 27 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment