KOCHA wa timu ya taifa ya Korea Kusini, Hong Myung-bo ameomba radhi wananchi wa taifa na kutangaza kujiuzulu wadhifa wake huo kutokana na nchi hiyo kutolewa mapema katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Brazil. Taarifa hizo zimekuja ikiwa imepita wiki toka makamu wa rais wa Chama cha Soka cha nchi hiyo-KFA Huh Jung-Moo kudai kuwa walikataa barua ya kujiuzulu ya Hong. Jung-Moo alidai kuwa wamemshawishi Hong kuingoza nchi hiyo kwa ajili ya michuano ya Kombe la Asia itakayofanyika nchini Australia mwaka ujao. Korea Kusini walimaliza katika nafasi ya mwisho katika kundi H katika michuano hiyo na kuambulia alama moja pekee katika mechi tatu walizocheza.

No comments:
Post a Comment