Thursday, July 10, 2014

SUAREZ KIROHO SAFI KUTUA BARCELONA.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez anakaribia kukamilisha rasmi uhamisho wake kutoka klabu ya Liverpool kwenda Barcelona baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya dili hilo linalikadiriwa kuwa thamani ya euro milioni 88. Makubaliano hayo yamekuja baada ya wiki nzima ya mazungumzo baina ya vilabu hivyo huku taarifa rasmi zikitarajiw akutolewa ndani ya siku chache zijazo. Inaaminika kuwa Suarez atafanyiwa vipimo vya afya kutoka kwa madaktari wa Barcelona akiwa nchi kwao Uruguay ambako ndipo alipokuwa toka nchi yake ienguliwe katika michuano ya Kombe la Dunia. Barcelona imefanikiwa kumnasa Suarez moja kwa moja baada ya kukubali kufikia dau lililowekwa katika mkataba wa mchezaji waliosaini Liverpol Desemba mwaka jana. Klabu hiyo inatarajiwa kuongezea fedha watakazopata kutokana na mauzo ya mshambuliaji wao Alexis Sanchez ambaye atahamia Arsenal baada ya klabu hiyo kukubali kutoa kitita paundi milioni 31.8.

No comments:

Post a Comment