Wednesday, January 13, 2016

DE BRUYNE ALITAKA KWENDA BAYERN KABLA YA MAN CITY - WAKALA.

WAKALA wa kiungo Kevin De Bruyne amedai mteja wake alikubali dili la kujiunga na Bayern Munich kabla ya kuamua kwenda Manchester City. Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alijiunga na City mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka jana kwa kitita kilichovunja rekodi ya klabu cha paundi milioni 55. Lakini sasa wakala wa kiungo huyo, Patrick De Koster amebainisha mteja wake huyo angeweza kwenda Bayern kama mabingwa hao wa Ujerumani wangelipa ada iliyotakiwa. De Koster amesema moyo wa De Bruyne ilikuwa bado unataka kuendelea kucheza katika Bundesliga ambapo aliibukia Werde Bremen na baadae kung’aa akiwa Wolfsburg. Wakala huyo aliendelea kudai kuwa ana uhakika De Bruyne angeishia Bayern kama klabu hiyo ingelipa dau lililohitajika.

No comments:

Post a Comment