Wednesday, January 13, 2016

RUFANI YA BARCELONA KWA SUAREZ YATUPWA.

RUFANI ya Barcelona kupinga Luis Suarez kufungiwa mechi mbili za michuano ya Kombe la Mfalme kwa tuhuma za kuanzisha vurugu katika korido baada ya mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Espanyol imekataliwa. Katika mchezo huo uliowakutanisha mahasimu wa jiji, Barcelona walishinda mabao 4-1 katika Uwanja wa Camp Nou lakini wachezaji walionekana kugombana wakiwa njiani kuelekea katika vyumba vyao baada ya kutoka uwanjani mpaka kufikia hatua ya kutenganishwa na watu wa usalama. Kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi Suarez alidaiwa kutoa maneno ya vipisho wakati wakiwa koridoni na kupelekea kutaka kushikana kabla hawajatenganishwa. Nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay anatarajiwa kuukosa mchezo wa maruadiano utakaofanyika baadae leo pamoja na mchezo war obo fainali kama wakifanikiwa kufika hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment