Friday, January 15, 2016

PAMOJA NA KUFUNGIWA MADRID YAPANGA KUFANYA KUFURU KIANGAZI.

KLABU ya Real Madrid inaripotiwa kuwaweka katika orodha yake ya usajili wa kiangazi nyota wa Ligi Kuu kama Harry Kane, Eden Hazard, David de Gea na John Stones wakati wakipambana kupinga adhabu ya kufungiwa kusajili. Madrid wamelimwa adhabu hiyo jana na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kufuatia kukutwa na hatia ya kukika sheria ya kusajili wachezaji wa kigeni walio chini ya umri wa miaka 18. Klabu hiyo ina matumaini rufani yao inaweza kusogeza mbele adhabu yao hiyo mpaka Januari mwakani hata kama wakishindwa. Atletico Madrid ambao wamepata adhabu kama hiyo, nao wameripotiwa kuwania kumrudisha tena Diego Costa, Vicente Calderon.

No comments:

Post a Comment