KLABU za Real Madrid na Atletico Madrid zimeonyeshwa kuchukizwa kufungiwa mwaka mmoja kusajili wachezaji wapya na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA jana, na kutangaza nia yao ya kukata rufani. Klabu zote mbili zimelimwa adhabu hiyo kufuatia kukiuka sheria ya usajili wa wachezaji wa kigeni wenye umri wa chini ya umri wa miaka 18. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wake, Madrid wamedai kuwa watapinga umuzi huo wa FIFA katika mamlaka zote za soka. Naye rais wa Atletico Enrique Cerezo amesema pamoja na kuwa wanaweza kukabiliana na adhabu hiyo kutokana na kikosi walichonacho lakini watakata rufani kwasababu wanaamini hawakutendewa haki katika maamuzi hayo. Real na Atletcio pia wamepigwa faini ya dola 358,000 na 895,000 na kupewa siku tisini kurekebisha suala hilo.

No comments:
Post a Comment