KLABU za Real Madrid na Atletico Madrid zimefungiwa kusajili wachezaji wapya kwa misimu miwili ijayo. Klabu hizo zimelimwa adhabu hiyo na Shirikihso la Soka Duniani-FIFA kufuatia kukutwa na hatia ya kusajili wachezaji walio chini ya umri kinyume na utaratibu. Adhabu hiyo haitaathiri usajili wao wa kipindi cha Januari ambao unamalizika mwishoni mwa mwezi huu. Mbali na adhabu hiyo Atletico wamelimwa faini ya paundi 622,000 wakati Madrid wao wameamriwa kulipa paundi 249,000. Timu hizo zinaweza kusajili wachezaji katika kipindi hiki lakini baada ya hapo hawataweza tena mpka vipite vipindi viwili vya usajili.

No comments:
Post a Comment