KLABU ya Arsenal inadaiwa kutenga kitita cha fedha kwa ajili ya kumuwania mshambuliaji wa kimataifa wa Nigeria Sadiq Umar. Taarifa kutoka katika magazeti ya Italia zinadaia kuwa klabu ya AS Roma imeshakataa ofa ya awali ilitolewa na Arsenal kwa ajili ya chipukizi huyo mwenye umri wa maiak 19 ambayo inakadiriwa kufikia paundi milioni 10. Roma wanadaiwa kuwa wataweza kusikiliza ofa kwa ajili ya nyota huyo kama Arsenal wataongeza dau zaidi ya lile walilotoa awali. Inadaiwa kuwa Roma wanataka walau paundi milioni 11.8 ili waweze kumuachia chipukizi huyo.

No comments:
Post a Comment