Sunday, March 13, 2016

FERGUSON AIPIGIA CHAPUO LEICESTER KUTWAA TAJI LA LIGI KUU.

MENEJA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amedai kuwa Leicester City wanaweza kushinda taji la Ligi Kuu huku wakiwa bado na mechi tatu mkononi. Leicester wanaonolewa na Claudio Ranieri wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano huku kukiwa kumebaki mechi tisa, ingawa Tottenham Hotspurs wanaweza kupunguza pengo hilo kama wakishinda mchezo wao dhidi ya Aston Villa baadae leo. Lakini Ferguson ambaye aliiongoza United kunyakuwa mataji 13 ya ligi katika kipindi cha miaka 27 aliyokaa Old Trafford anaamini Leicester wanaweza kupambana na kikwazo chochote msimu huu. Akihojiwa Ferguson amesema anadhani Leicester wanaweza kuwa mabingwa msimu huu kwasababu wameonyesha kuwa imara na uwezo wa kuifunga timu yeyote ile.

No comments:

Post a Comment