KOCHA wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga anapendelea zaidi nyota wa Barcelona Neymar kucheza michuano ya Olimpiki badala ya ile ya Copa America. Neymar mwenye umri wa miaka 24 anategemewa kuchagua moja kati ya michuano hiyo miwili ambayo yote inatarajiwa kufanyika baada ya ratiba ngumu ya msimu ya Barcelona kumalizika. Dunga ambaye anainoa timu ya wakubwa na ile ya vijana chini ya miaka 23, anatarajiwa kukutana na uongozi wa Barcelona kujadili jinsi atakavyomtumia Neymar. Akihojiwa Dunga amesema ni vigumu kuchagua lakini anadhani swala muhimu ni medali ya olimpiki ambayo Brazil haijawahi kunyakuwa.

No comments:
Post a Comment