Wednesday, March 9, 2016

LIGI KUU YAPITISHA OMBI LA BILIONEA WA ZAMANI WA ARSENAL KUWEKEZA EVERTON.

KLABU ya Everton imetangaza kuwa Ligi Kuu imepitisha ombi la bilionea Farhad Moshiri kuwekeza katika timu hiyo. Moshiri ambaye anakadiriwa kuwa na utajiri wa paundi bilioni 1.3 kwa mujibu wa jarida maarufu la Forbes, anatarajiwa kumiliki hisa asilimia 49.9 za klabu hiyo. Moshiri ambaye ni mwanahisa wa zamani wa Arsenal anatarajiwa kufanya kazi sambamba na Bill Kenwright na Jon Woods wamiliki wengine wa hisa zilizobakia za klabu hiyo. Everton ilikubali kumuuzia hisa Moshiri Februari 27 baada ya bilionea huyo kuamua kuuza hisa zake alizokuwa akimiliki katika klabu ya Arsenal.

No comments:

Post a Comment