GOLIKIPA wa zamani wa Manchester United Edwin van der Sar anatarajia kurejea tena uwanjani akiwa na umri wa miaka 45 kuitumikia klabu yake ya utotoni ya VV Noorwijk kwa mara nyingine. Mchezo wa mwisho kwa golikipa huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi ulikuwa mwaka 2011 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo United walitandikwa mabao 3-1 na Barcelona, lakini aliendelea kuwa mjumbe wa klabu hiyo ya Uholanzi ambayo ghafla imekumbwa na balaa na majeruhi. Kufuatia golikipa wake Mustafa Mare Zine kuumia, Noordwijk ilituma maombi Chama cha Soka cha nchi hiyo-KNVB ya kutaka Van de Sar aruhusiwe kucheza katika mechi yao dhidi ya Jodan Boys Jumamosi hii na kukubaliwa. Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Pieter Vink alithibitisha taarifa hizo na kumshukuru Van der Sar.

No comments:
Post a Comment