MAHAKAMA nchini Hispania imekubali rufani kutoka rais wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu na rais wa zamani Sandro Rosell kuhusiana na tuhuma za ukwepaji kodi uliotokana na usajili wa Neymar. Mabingwa hao wa Ulaya walithibitisha taarifa hizo jana usiku kupitia mtandao wake wakieleza kuwa sio Bartomeu wala Rosell ambaye atapanda mahakamani kuhusiana na tuhuma hizo. Barcelona pia imeshafishwa kuondolewa mashitaka ya kodi katika kesi hiyo baada ya rufani yao hiyo. Taarifa ya klabu imedai kuwa uamuzi huo unamanisha kuwa Barcelona, Bartomeu na Rosell wote sio watuhumiwa tena katika kesi hiyo.

No comments:
Post a Comment