KIUNGO wa Barcelona, Javier Mascherano amedai kutojali ukame wake wa mabao na kusisitiza kukataa kupiga penati ili asivunje rekodi yake hiyo. Mascherano hajafunga bao katika mechi 200 za mashindano alizocheza toka ajiunge na klabu hiyo mwaka 2010. Kiungo huyo wa kimataifa wa Argentina hajafunga bao toka Machi mwaka 2008 wakati akiichezea Liverpool waliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Reading. Mchezaji mwenzake Gerrard Pique amesema Mascherano alikataa kupiga penati katika ushindi wa mabao 5-1 waliopata dhidi ya Rayo Vallecano wiki iliyopita ambapo badala yake alipiga Luis Suarez na kukosa.

No comments:
Post a Comment