MAWAKILI wa mshambuliaji nyota wa Real Madrid, Karim Benzema wamedai kuwa mteja wao yuko huru kuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa katika michuano ya Euro 2016 baada ya zuio la kisheria alilowekewa kutokana na kutuhumiwa kuhusika na kashfa ya mkanda wa ngono kuondolewa. Chini ya zuio hilo, Benzema alikatazwa kukutana na mchezaji mwenzake wa kimataifa wan chi hiyo Mathieu Valbuena ambaye ndio alikuwa akihusiaka na kashfa hiyo. Lakini mahakama ya rufani imeondoa zuio hilo na kumruhusu Benzema kujihusisha na kikosi cha timu ya taifa kama ilivyo kwa Valbuena kama wawili hao watachaguliwa kushiriki michuano hiyo itakayofanyika katika ardhi yao. Mawakili wa Benzema wamesema kazi yao wamemaliza na sasa uamuzi wa kama mteja wao awepo katika michuano ya Euro 2016 hauko chini yao tena. Kocha wa Ufaransa, Didier Dischamps alimsimamisha Benzema mwenye umri wa miaka 28 kukitumikia kikosi cha nchi hiyo baada ya kuwekwa chini uchunguzi kuhusiana na suala hilo Novemba mwaka jana.

No comments:
Post a Comment