Wednesday, March 9, 2016

EBOUE ATUA SUNDERLAND.

KLABU ya Sunderland imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa Arsenal Emmanuel Eboue kwa mkataba wa muda mfupi. Beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amekuwa akifanya mazoezi na Sunderland katika kipindi cha wiki kadhaa na sasa klabu imethibitisha kumchukua kwa msimu wote uliosalia. Eboue mwenye umri wa miaka 32 amekuwa mchezaji huru kufuatia kuondoka Galatasaray mwishoni mwa msimu uliopita akiwa ameshinda mataji matatu ya ligi katika kipindi cha miaka minne aliyokuwa Uturuki. Sunderland imeamua kumchukua Eboue ili kuongeza uzoefu katika kikosi chake kufuatia kuitumikia Arsenal kwa zaidi ya mechi 100 huku akiisaidia kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment