MKURUGENZI wa michezo wa Borussia Dortmund, Michael Zorc amepuuza taarifa zinazomhusisha mshamabuliaji wao Pierre-Emerick Aubameyang na tetesi za kwenda Real Madrid majira ya kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Gabon amekuwa akihusishwa na tetesi hizo za kwenda Santiago Bernabeu mwishoni mwa msimu kwa dau kubwa ambalo linafikia euro milioni 100. Tetesi hizo zimezuka kutokana na kiwango bora ambacho Aubameyang ameendelea kukionyesha msimu huu akiwa ameshafunga mabao 22 katika mechi 24 za Bundesliga alizocheza. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Zorc amesema hakuna ofa yeyote wala maombi yalitolewa hivyo tetesi hizo hazina maana yeyote.

No comments:
Post a Comment