KLABU ya Atletico Madrid kuanzia mwakani inatarajiwa kucheza mechi zake za nyumbani katika Uwanja wa Wanda Metropolitano baada ya jina hilo jipya la uwanja wao kuthibitishwa mapema leo. Uwanja huo mpya umepewa jina la uwanja wa zamani waliotumia kabla ya kuhamia huu wanaotumia sasa wa Vicente Calderon pamoja na wawekezaji wa China. Atletico walicheza katika Uwanja wa Metropolitan kuanzia mwaka 1923 mpaka 1966 kabla ya kuhamia katika uwanja wanaotumia hivi sasa uliopewa jina la rais wa zamani Vicente Calderon. Akihojiwa katika uzinduzi huo, mshambuliaji wa Atletico Fernando Torres amesema alifahamu kutoka kwa babu yake kuhusu Metropolitano, ni jina zuri. Atletico pia watabadilisha muonekano wa nembo yao pindi watakapohamia katika uwanja wao huo mpya.

No comments:
Post a Comment