Friday, December 9, 2016

HAKUNA MCHEZAJI ANAYEZIDI KLABU - WENGER.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ana uhakika Santi Cazorla ataisaini mkataba mpya lakini amesisitiza kuwa klabu hiyo ni kubwa kuliko mchezaji mmoja au wawili kufuatia tetesi zinazoendelea juu ya mustakabali wa Mesut Ozil na Alexis Sanchez. Nyota hao wote wamebakisha mkataba wa miezi 18 katika miakataba yao, na kumekuwa na taarifa kuwa wanataka kupandishiwa mishahara yao ili wafikie viwango vya nyota wengine Ligi Kuu. Ozil kwasasa analipwa kitita cha paundi 140,000 kwa wiki huku Sanchez yeye akipokea paundi 130,000. Wenger tayari ameshathibitisha kuwa hana mpango wowote wa kuwauza nyota majira ya kiangazi hata kama wakikataa kuongeza mikataba yao katika mazunguko yanayoendelea hivi sasa. Akihojiwa Wenger amesema tayari mazungumzo na Cazorla yamefikia pazuri na amekubalia kuongeza mkataba wake. Hata hivyo, Wenger aliongezea kuwa klabu hiyo kubwa na mchezaji mmoja au wawili hawezi kuweka tofauti yeyote, jambo la muhimu hivi ni kwamba wako katika hali nzuri kiuchumi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

No comments:

Post a Comment