Sunday, December 11, 2016

BOMU LAUA 38 NJE YA UWANJA WA BESIKTAS.

MABOMU mawili yaliyolenga kuwashambulia maafisa wa polisi nje ya uwanja wa soka jijini Instabul, yameua watu 38 na kujeruhi wengine kadhaa. Gari lililokuwa na bomu liligonga gari la polisi na mtu wa kujitoa muhanga alijilipua katika kitendo kilichofanyika kwa haraka jana usiku. Mlipuko huo ulitokea karibu na uwanja wa klabu ya Besiktas, saa mbili baada ya kumalizika kwa mchezo na watu kumi wanaripotiwa kukamatwa kufuatia tukio hilo. Maofisa wa usalama wamesema watu 30 kati ya waliouawa ni maofisa wa polisi huku watu wengine 115 wakijeruhiwa na kupatiwa matibabu hospitali.

No comments:

Post a Comment