Sunday, December 11, 2016

ZIDANE AENDELEA KUPANGUA REKODI ZA MADRID TARATIBU.

KLABU ya Real Madrid jana imefanikiwa kuweka rekodi mpya ya kutofungwa katika mechi 35 za mashindano yote walizocheza baada ya kuibugiza Deportivo La Coruna kwa mabao 3-2. Katika mchezo huo Deportivo walionekana kama wanngeweza kuwazuia Madrid kufikia rekodi yao hiyo baada ya kuongoza kwa mabao mawili mapema lakini walishindwa kuwazuia mabingwa hayo wa Ulaya pamoja na kumpumzisha nyota wao Cristiano Ronaldo. Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane sasa inakuwa imeipita rekodi ya kutofungwa mechi 34 iliyokuwa imewekwa katika msimu wa 1988-1989 na kocha Mholanzi Leo Beenhakker. Zidane alifanya mabadiliko katika kikosi chake akipumzisha Ronaldo, Karim Benzema na Luka Modric kwa ajili ya kujiandaa na safari yao kuelekea nchini Japan kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.

No comments:

Post a Comment