Sunday, December 11, 2016

SEATTLE SOUNDERS MABINGWA WA MLS.

KLABU ya Seattle Sounders imefanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu ya Marekani-MLS kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa Toronto FC kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-4. Beki Roman Torres ndiye aliyefunga penati ya ushindi baada y timu hizo kushindwa kufungana katika muda wa kawaida na ule wa nyongeza. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, meneja wa Seattle, Brian Schmetzer alikipongeza kikosi chake kufuatia kutwaa taji hilo. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa mpaka kufikia hatua ya matuta mchezo ungeweza kwenda popote lakini anashukuru ni wao ndio walioibuka kidedea mwishoni.

No comments:

Post a Comment