KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Gilberto Silva amejiuzulu wadhifa wake kama mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Panathinaikos baada ya kupita miezi saba. Silva alijiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu Mei mwaka huu baada ya kuichezea kuanzia mwaka 2008 mpaka 2011. Rais wa Panathiniakos Yannis Alafouzos alimpa Gilberto ofa ya kuwa balozi ili aendelee kuwepo klabuni hapo lakini mwenyewe alikataa ofa hiyo. Akihojiwa mapema Octoba, Gilberto mwenye umri wa miaka 40 alibainisha kuwa alipokuwa mchezaji ilikuwa kazi rahisi zaidi kuliko nafasi ya ukurugenzi wa ufundi. Gilberto alianza soka lake katika klabu ya America Mineiro mwaka 1997 na pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Arsenal kilichotwaa taji la Ligi Kuu bila kufungwa mwaka 2004.

No comments:
Post a Comment