WAKALA wa meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema mteja wake huyo alilipa zaidi ya kodi ya euro milioni 26 wakati alipoondoka nchini Hispania kuanzia 2010 hadi 2013. Taarifa hizo ziliwekwa hadharani jana na Gestifute, kampuni ambayo inasimamiwa na wakala wa Mourinho, Jorge Mendes. Kampuni hiyo ya Ureno ilitoa taarifa za kodi ya meja wake huyo baada ya vyombo vya habari vya Ulaya kuchapisha madai kuwa kumekuwa na mchezo wa kukwepa miongoni kwa baadhi ya wachezaji wkaubwa na makocha wakiwemo Mourinho, Cristiano Ronaldo na Mesut Ozil. Gestifute ambao pia ndio wanaomsimamia Ronaldo tayari walishatoa taarifa zinazoonyesha kuwa mamlaka za kodi nchini Hispania walishawakagua wateja wao hao na kuona hawana matatizo yeyote kwenye ulipaji wa kodi.

No comments:
Post a Comment