KLABU ya Middlesbrough inadaiwa kutaka kiasi kikubwa cha paundi milioni 35 kwa ajili ya Ben Gibson ili kuitisha Chelsea. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 amekuwa katika kiwango bora msimu huu akisaidia vyema safu ya ulinzi ya klabu hiyo. Meneja wa Chelsea Antonio Conte bado anataka kuimarisha safu yake ya ulinzi katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari lakini sasa inadaiwa kuna uwezekano wa kushindwa kumuwania Gibson kutokana na bei yake. Everton nao pia wanadaiwa kutaka kumuwania Gibson ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano na Middlesbrough mapema mwaka huu.

No comments:
Post a Comment