Friday, August 12, 2011

"NAWEZA KUWA BORA KULIKO MESSI." NEYMAR


MSHAMBULIAJI wa Brazil Neymar anafikiri kuwa anaweza kuwa bora kama alivyo nyota wa Barcelona Leonel Messi na ikiwezekana kumzidi Muagentina huyo huko mbeleni.

Neymar (19) anayekipiga Santos amehusishwa na timu kadhaa za Ulaya zilizokuwa zinammezea mate zikiwemo timu za Real Madrid na Barcelona.

Kiwango alichokionyesha mshambuliaji huyo kimeonekana kuwakosha Pele na Kaka ambapo Neymar mwenyewe naye alionekana kujiamini kutokana na kiwango chake hicho na alipoulizwa anajifananishaje mwenyewe na Messi alijibu "Naweza kuwa mchezaji mkubwa kama yeye au zaidi yake nina uhakika na hilo."

Wakati alipoulizwa kuhusu uwezekano wa kuhama kutoka katika klabu yake ya sasa Santos alilikwepa swali hilo kwa kujibu, "Siongelei kuhusu mustakabali wangu huko mbele. Mawazo yangu yapo kwa timu ya Taifa na Santos, halafu tutaona itakuwaje, sio kitu nachokihofia au kukiongelea."

Neymar ndiye aliyeifungia Brazil bao la kufuta machozi wakati ilipochapwa mabao 3-2 na Ujerumani katika mchezo wa kirafiki Jumatano.

No comments:

Post a Comment