![]() |
Orlando Silva |
WAZIRI wa Michezo wa Brazil Orlando Silva ambaye alikuwa na kazi ya kuandaa Kombe la Dunia 2014 amejiuzulu wadhifa wake huo kwa tuhuma za rushwa zinazomkabili ikiwa ni siku moja toka uchunguzi wa tuhuma hizo uanze.Silva ni waziri wa tano katika serikali ya Rais Dilma Rousseff ndani ya miezi mtano kulazimika kujiuzulu baada kutuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha za uma.Waziri huyo amesema katika ripoti yake kwa waandishi baada ya kuchukua uamuzi huo kuwa ameachia wadhifa wake huo ili kulinda heshima yake na kwamba anaondoka akiw ametimiza wajibu wake.Silva alikataa tuhuma hizo zinazomkabili na akusema kuwa ukweli juu ya suala hilo utajitokeza.
No comments:
Post a Comment