Friday, July 6, 2012

AFCON QUALIFIER DRAW.

WAWAKILISHI pekee waliobakia Afrika Mashariki katika kinyang’anyiro cha kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika itakayofanyika nchini Afrika Kusini mwakani nchi, ya Uganda imepangwa na mabingwa wa Afrika Zambia katika ratiba iliyopangwa jana. Katika michezo hiyo ambayo itachezwa nyumbani na ugenini Uganda watawafuata Zambia nyumbani kwao katika mchezo wa kwanza kabla ya kuwakaribisha jijini Kampala mabingwa hao katika mchezo wa marudiano ambapo timu itakayofanikiwa kushinda katika michezo hiyo miwili itakuwa imekata tiketi ya kushiriki michuano hiyo. Katika ratiba hiyo Ivory Coast ambao walishika nafasi ya pili katika michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika mapema mwaka huu imepangwa na Senegal wakati Afrika ya Kati ambao waliiondosha Misri wako katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kupangwa na Burkina Faso. Nchi nyingine ni Ghana itapambana na Malawi, Nigeria na Liberia, Mali na Botswana, Zimbwabe na Angola, Cape Verde na Cameroon, Msumbiji na Morocco, Sierra Leone na Tunisia, Guinea na Niger, Sudan na Ethiopia, Libya na Algeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Equatorial Guinea wakati Gabon watachuana na Togo.

No comments:

Post a Comment