NCHI ya Benin imejiweka katika hatari ya kufungiwa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kujishughulisha na masuala ya soka kama watashindwa kutii amri ya Kamati ya masuala ya Dharura ya shirikisho hilo inayowataka kumrejesha madarakani aliyekuwa rais wa Shirikisho la Soka la nchini hiyo-FBF, Anjorin Moucharafou ambaye aliondolewa kwa amri ya makahama ya rufani. Katika taarifa iliyotumwa na kamati hiyo kwenda shirikisho la soka la nchi hiyo, imesema kuwa maamuzi yaliyofanywa na mahakama ya rufani ni ukiukwaji wa wazi wa ibara ya 13 na 17 ya sheria za FIFA ambazo zinahitaji wanachama wake kusimamia mambo yao kwa kujitegemea bila kuingiliwa na chama chochote cha tatu. Taarifa hiyo imesema kuwa inasubiri mahakama ya rufani itengue adhabu yake hiyo ili iweze kutoa uwamuzi wa mwisho na kama wakishindwa kufanya hivyo FBF itafugiwa na FIFA Kwa mujibu wa kamati hiyo, kama Benin watafungiwa hiyo itamaanisha wachezaji, viongozi, vilabu na wajumbe wengine wa FBF watanyimwa fursa ya kujishughulisha na mambo yoyote ya michezo ndani ya bara hili na kimataifa.
Wednesday, July 25, 2012
BENIN HATARINI KUFUNGIWA NA FIFA.

No comments:
Post a Comment