Friday, July 6, 2012
SILVA, HULK WAJUMUISHWA KIKASI CHA BRAZIL CHA OLIMPIKI.
BEKI wa klabu ya AC Milan Thiago Silva na Mshambuliaji wa klabu ya Porto, Hulk wamejumuishwa katika kikosi cha Brazil ambacho kitajaribu kunyakuwa medali ya dhahabu kwa mara ya kwanza katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London, Uingereza. Beki wa Real Madrid Marcelo naye pia amejumuishwa katika kikosi hicho cha wachezaji 18 kwa wachezaji wenye umri mkubwa kilichoteuliwa na kocha Mano Manezes ambaye atajaribu kushinda medali ya dhahabu kwenye michuano hiyo ikiwa ni taji pekee la kimataifa ambalo nchi hiyo haijalinyakuwa. Brazil ni mojawapo ya timu ambazo zitapleka wachezaji wake nyota katika michuano hiyo na itakuwa timu itakayopewa nafasi ya kunyakuwa medali ya dhahabu ambapo wachezaji wengi watakaokuwemo kwenye kikosi hicho wanategemewa kuwemo katika kikosi cha michuano ya Kombe la Dunia 2014 pia. Kikosi kamili cha wachezaji wa timu hiyo na vilabu wanavyotoka ni pamoja na makipa: Rafael-Santos, Neto-Fiorentina, beki: Alex Sandro-FC Porto, Marcelo-Real Madrid, Danilo-FC Porto, Rafael-Manchester United, Bruno Uvini-Sao Paulo, Juan-Inter Milan, Thiago Silva-AC Milan. Wengine viungo: Romulo-Spartak Moscow, Sandro-TottenhamHotspurs, Paulo Henrique Ganso-Santos, Oscar-Internacional, Lucas-Sao Paulo, washambuliaji: Alexandre Pato-AC Milan, Hulk-FC Porto, Leandro Damiao-Internacional, Neymar-Santos.
No comments:
Post a Comment