Friday, September 7, 2012
BOLT, BLAKE KUMALIZIA MSIMU BRUSSELS.
WANARIADHA nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica, Usain Bolt na Yohane Blake wanatarajiwa kumaliza msimu wa mwisho wa michuano ya Diamond League jijini Brussels. Hatahivyo wanariadha hao hawatachuana katika mbio za leo baada ya Bolt kuamua kukimbia mbio za mita 100 na Blake atakimbia za mita 200. Blake ambaye alikimbia kwa kutumia muda wa sekunde 19.26 katika uwanja huo mwaka uliopita, amepania kukimbia muda mwingine wa haraka zaidi nchini Ubelgiji. Akizungumza kuhusiana na michuano hiyo Blake ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu katika mbio za kupokezana vijiti za mita 400 pamoja na medali ya fedha katika mbio za mita 100 na 200 katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini London mwaka huu, amesema kuwa amejiandaa vyema na yuko tayari kuvunja rekodi yake.

No comments:
Post a Comment