Saturday, February 9, 2013

WENGER AITAKA UEFA KUCHUKUA VIPIMO VYA DAMU BADALA YA MKOJO ILI KUWABAINI WACHEZAJI WADANGANYIFU.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai ameliomba mara nyingi Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuangalia uwezekano wa kutumia vipimo vya damu ili kuwapa wachezaji ambao wanatumia dawa za kuongeza nguvu kweny soka. UEFA inatumia vipimo vya mkojo ili kudhibiti suala hilo hivi sasa lakini Wenger anafikiri vipimo hivyo havitoshi ili kuwakamata wachezaji wadanganyifu wanaotumia dawa za kuongeza nguvu. Wenger amesema hafikirii kama UEFA wanafanya kazi ya kutosha kudhibiti suala hilo kwasababu ni ngumu kwake kuamini kuwa wachezaji zaidi ya 740 wanaopimwa katika michuano ya Kombe la Dunia halafu unakuta hakuna hata mchezaji mmoja aliyeshikwa kwa udanganyifu. Kocha huyo anasema mara nyingi amekuwa akiitaka UEFA kufanya uchunguzi wa ndani zaidi ili kuwabaini wachezaji ambao hufanya udanganyifu kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu katika mikutano mbalimbali ya shirikisho hilo jijini Geneva, Switzerland. UEFA inajipanga kubadilisha sheria za upimaji ili kudhibiti tatizo la utumiaji dawa za kuongeza nguvu lakini inaweza kupata wakati mgumu kwasababu za kimaadili. 

No comments:

Post a Comment