
Saturday, March 16, 2013
AUSTRALIA GRAND PRIX: GROSJEAN AONGOZA FINAL PRACTICE.
DEREVA wa timu ya Lotus Romain Grosjean amefanikiwa kuendesha kwa kasi zaidi na kumzidi Fernando Alonso wa timu ya Ferrari katika majaribio ya mwisho katika mvua kabla ya kuanza kwa mashindano ya kwanza msimu huu ya Australia Grand Prix. Mfaransa huyo alimpita Alonso kwa sekunde 0.071 muda mfupi kabla mvua kubwa haijaanza kunyesha katika barabara za Albert Park kunakofanyika mashindano hayo. Katika mbio hizo za mwisho za majaribio bingwa wa Dunia Sebastian Vettel alitoka nje ya barabara baada ya gari lake kupata matatizo ambapo fundi mkuu wa timu ya Red Bull alikika akimtaka Vettel kutoka nje ya barabara baada ya gari lake kuharibika. Lakini ofisa mkuu wa timu hiyo baadae adai kuwa kuna baadhi ya vyombo vya umeme katika gari hilo vilishinwa kufanya kazi sawasawa kwa kutoa taarifa zisizo sahihi. Mashindano hayo ambayo ilikuwa yaendelee tena leo yalisimamishwa mpaka Jumapili baada ya mvua kubwa kunyesha katika jiji la Melbourne hivyo kuhatarisha usalama wa madereva wanashiriki mbio hizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment