Saturday, March 16, 2013

D'HOOGHE APINGA QATAR KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2022 KATIKA KIPINDI CHA KIANGAZI.

OFISA wa afya wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Michel D’Hooghe amepinga vikali michuano ya Kombe la Dunia 2022 kuandaliwa katika kipindi cha joto la kiangazi katika nchi ya Qatar ambayo sehemu kubwa ni jangwa. Ofisa huyo alitoa kauli hiyo wakati wa mdahalo uliofanyika Ijumaa iliyopita unaohusu Qatar kama iruhusiwe kuandaa michuano hiyo katika kipindi cha kawaida cha mwezi June au wahamishe katika mizi ambayo hali ya hewa itakuwa imepoa kidogo. Katika mdahalo huo ofisa huyo alidai kuwa hata kama mechi na mazoezi vitakuwa vikifanyika katika vipoza hewa vyenye nyuzi joto 21, maelfu ya mashabiki na maofisa wengine watakaokuwa wakifuatilia michuao hiyo ya mwezi mzima watakuwa wakipambana na joto hilo kali katika kipindi hicho. Rais wa FIFA Sepp Blatter amedai kuwa kwasasa tatizo hilo bado halijatatuliwa mpaka watakapopata ushahidi wa kitabibu kama kweli joto litakalokuwepo kipindi hicho lina adhari zozote za kiafya kwa wachezaji na mashabiki watakaokuwa huko.

No comments:

Post a Comment