Monday, March 18, 2013
INTER KITANZINI TENA KWA VITENDO VYA KIBAGUZI.
KLABU ya Inter Milan ya Italia imeshitakiwa kwa tabia za kibaguzi za mashabiki walizozionyesha wakati wa mchezo wa Europa League dhidi ya Tottenham Hotspurs uliochezwa wiki iliyopita. Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA pia limeituhumu klabu hiyo kwa kukosa ushirikiano na kurusha vitu mbalimbali wakati wa mchezo huo ambapo kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa April 19 mwaka huu. Taarifa za mashabiki waliokuwa wakishangilia kwa kupiga kelele za nyani zilitolewa wakati wa mchezo huo uliochezwa Alhamisi iliyopita ambapo Spurs walifanikiwa kusonga mbele kwa bao la ugenini pamoja na kufungwa mabao 4-1. Inter tayari wameshapigwa faini ya paundi 43,000 na maofisa wa Ligi Kuu nchini Italia msimu huu baada ya mashabiki wake kukutwa na hatia ya kuwafanyia vitendo vya kibaguzi wachezaji wa zamani wa klabu hiyo Mario Balotelli na Sulley Muntari ambao wote kwasasa wanacheza AC Milan.
No comments:
Post a Comment