Saturday, March 16, 2013

MURRAY ABANDULIWA MICHUANO YA WAZI YA BNP PARIBAS, INDIAN WELLS.

MCHEZA nyota kutoka Uingereza, Andy Murray ametolewa nje ya michuano ya wazi ya BNP Paribas baada ya kukubali kufungwa na Juan Martin del Potro wa Argentina huko Indian Wells, California. Del Potro alifanikiwa kumuengua Murray kwa kumfunga seti tatu zenye alama za 6-7 6-3 6-1 na sasa atakutana na Novak Djokovic katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo. Djokovic raia wa Serbia ambaye anashika namba moja katika katika orodha za ubora duniani alitinga hatua hiyo kwa kishindo baada ya kumuondosha Jo-Wilfried Tsonga kwa 6-3 6-1 akitumia muda wa dakika 53 pekee. Mara baada ya mchezo huo Murray ambaye anashika namba tatu katika orodha za ubora amekiri kwamba ulikuwa mchezo mgumu kwani mpinzani wake alikuwa akicheza kama mtu ambaye ameshinda mechi nyingi. Katika nusu fainali nyingine itakayochezwa leo Rafael Nadal atachuana na Tomas Berdych baada ya mhispania huyo kumng’oa Roger Federer katika hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment