Saturday, March 16, 2013
RAIS CBF MARIA MARIN MATATANI NCHINI BRAZIL.
Rais wa Shirikisho la Soka nchini Brazil-CBF, Jose Maria Marin anatatarajiwa kuanza kuhojiwa baada ya kuhisiwa kuwa na uhusiano na kifo cha mwandishi wa habari Vladimir Herzog. Herzog alitupwa jela na baadae kufariki mwaka 1975 wakati wa kipindi cha utawala wa kidikteta uliokuwa ukiongozwa na jeshi nchini Brazil. Katika kipindi hicho, Marn alikuwa Gavana wa jimbo la Sao Paulo na baada ya nguli wa soka wa zamani wan chi hiyo Romario kuomba kesi hiyo kusikilizwa, mwanasiasa Maria do Rosario ameruhusu suala hilo kufanyiwa uchunguzi upya. Do Rosario adai anadhani mtu yoyote ambaye amehusika kwa namna moja au nyingine katika kusababisha kifo cha mtu fulani, kuteswa au kupotea kwa mtu huyo hastahili kuwa mfano wa kuigwa nchini Brazil. Kwasababu mtu kama huyo anakuwa amekiuka haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment