Thursday, April 4, 2013

BAADA YA TEVEZ, NASRI NAYE ALAMBWA ADHABU KWA UZEMBE BARABARANI.

KIUNGO wa Manchester United, Samir Nasri amefungiwa kuendesha kwa kipindi miezi sita kwasababu ya kushindwa kulipa faini baada ya kukutwa akiendesha kwa mwendo kasi na gari lake. Adhabu hiyo imekuja baada ya mchezaji mwenzake Carlos Tevez kupewa siku 250 za kuhudumia jamii na pia kufungiwa miezi sita kwakutokuwa na bima. Nasri mwenye umri wa miaka 25 alipigwa faini ya paundi 1,900 lakini alifanikiwa kuiepuka baada ya kuandika barua kuwa hakujua kwamba gari lake aina ya Marcedes lilikuwa limekamatwa na kamera za barabarani kwamba lilizidisha mwendo katika matukio matatu tofauti. Lakini baadae polisi walikata rufani kuhusiana na suala hilo na kumuangushia adhabu hiyo kiungo huyo ingawa bado amepewa nafasi ya kukata rufani kama ataona hakutendewa haki.

No comments:

Post a Comment