Thursday, April 4, 2013

OLYMPIQUE MARSEILLE YAOMBA RADHI KWA NIABA YA BARTON.

KLABU ya Olympique Marseille na Joey Barton wameomba radhi kwa mchezaji Thiago Silva na klabu ya Paris Saint-Germain baada ya kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza kumtolea maneno ya kashfa mchezaji huyo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter. Katika taarifa iliyotolewa katika mtandao wa Marseille, klabu hiyo pamoja na kiungo huyo mtukutu walimuomba radhi Silva na klabu yake kwa maneno yasiyokuwa ya kiungwana ambayo yalitumwa na Barton katika twitter. Pia klabu hiyo ilimtaka Barton kumaliza tofauti zilizopo baina yao ambazo zimepelekea mpaka kurushiana na maneno ya kufedhehesha. PSG ilitishia kumchukulia hatua Barton kwa kauli yake ya kudhalilisha aliyotoa kwenda kwa Silva akimfananisha na mwanamke mnene kauli ambayo pia ilingwa vikali na wanaharakati mashoga.

No comments:

Post a Comment