
Thursday, April 4, 2013
ARSENAL WASABABISHA VURUGU.
KLABU ya Arsenal ya Argentina imejikuta ikipambana na mkono wa sheria baada ya vurugu zilizohusisha maofisa wa polisi wakati wa mchezo wa Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini maarufu kama Copa Libertadores jana. Katika mchezo huo klabu ya Atletico Mineiro ya Brazil ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Arsenal lakini wakati wachezaji wa timu hiyo Argentina wakijaribu kuwafuata waamuzi mara baada ya kipenga cha mwisho walikutana na polisi waliowazuia na kusababisha rabsha kubwa. Mmoja wa maofisa wa polisi aliyejitambulisha kwa jina la Claudia Romaualdo amesema wakati wakijaribu kujipanga ili kuwahakikishia usalama wachezaji wa timu ngeni kwenda kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo ghafla bila ya kutegemea wachezaji hao walianza kuwashambulia huku mchezaji mmoja akimpiga teke la kifuani. Ofisa huyo amesema lilitokea linasikitisha na sio suala la kimichezo kwani sheria zao zinapovunjwa hawana budi kuchukua hatua zinazostahiki. Wachezaji wanne wa Arsenal wanashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano baada ya klabu kuzuiwa kuondoka uwanjani mpaka wahusika wa vurugu hizo wapatikane. Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Atletico Mineiro, Eduardo Maluf ameviambia vyombo vya habari vya nchi hiyo kuwa chumba cha kubadilishia nguo walichokuwa wakitumia wachezaji wa Arsenal kimeharibiwa vibaya na wataiomba klabu hiyo kuwalipa gharama ya vitu vilivyoharibiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment