
Thursday, April 4, 2013
WENGER AMTETEA WALCOTT.
MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekanusha madai ya wadau kuwa kiwango cha Theo Walcott kimeporomoka kutokana na kupewa mkataba mpya Januari. Winga huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akionyesha kiwango bora katika sehemu ya kwanza ya msimu akifunga mabao 10 katika mechi 18 alizocheza lakini toka akubali kusaini mkataba mpya nyota huyo amefunga bao moja katika mchezo dhidi ya Liverpool miezi miwili iliyopita. Hatahivyo, Wenger amesema haamini kama kushuka kiwango kwa nyota huyo vinahusiana na suala la kupewa mkataba mpya na kuongeza anadhani katika siku za karibuni atarejea katika hali yake ya kawaida. Wenger amesema kama mchezaji huyo angekuwa hajapewa mkataba mpya na kucheza chini ya kiwango watu pia wangesema tofauti hivyo cha muhimu ni mashabiki kumpa muda ili aweze kurejea katika kiwango chake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment