Friday, April 5, 2013
BARCELONA KUMSHTAKI STARK.
KLABU ya Barcelona imepeleka malalamiko Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA kuhusu mwamuzi Wolfgang Stark ambaye alichezesha mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris Saint Germain. Klabu hiyo inamlalamikia Stark kwa kukataa kusimamisha pambano baada ya Javier Marcherano na Jordi Alba walipogongana tukio ambalo liliwaacha wachezaji wote wakigaragara chini kwa maumivu. Barcelona pia haikufurahishwa na Stark kuruhusu bao la kusawazisha la Zlatan Ibrahimovic baada ya kuonekana kama ameotea. Msemaji wa Barcelona Toni Freixa amesema wameamua kupeleka malalamiko hayo baada ya kushangazwa na maamuzi yaliyokuwa yakitolewa na Stark katika michuano mikubwa kama ni wazi kabisa alikuwa hafuati kanuni zilizowekwa. Barcelona inatarajiwa kuikaribisha Paris Saint-Germain katika mchezo wa marudiano utakaopigwa katika Uwanja wa Nou Camp Jumatano ijayo.
No comments:
Post a Comment