
Friday, April 5, 2013
BAYERN NI SAWA NA BARCELONA NA REAL MADRID - MATRI.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Juventus ya Italia, Alessandro Matri anaamini kuwa klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani iko katika nafasi sawa na Barcelona na Real Madrid za Hispania kama timu bora barani Ulaya. Juventus ambao ni mabingwa wa Serie A walifungwa mabao 2-0 na Bayern katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na nyota huyo anategemea mchezo mgumu wa marudiano wiki ijayo. Matri amesema wamesikitishwa kwa kupoteza mchezo dhidi ya Bayern lakini pia wamegundua kuwa walikuwa wakicheza na timu ngumu ambayo ina uwezo sawa na Barcelona na Madrid. Nyota huyo amesema walijitahidi kucheza mchezo wao lakini hiyo haikutosha kwasababu walikubali kufungwa bao la mapema na anategemea mchezo mgumu wa marudiano ingawa amedai kila kitu kinawezekana katika mchezo wa soka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment