Friday, April 5, 2013

LIBYA SASA SHWARI.

LIBYA kwa mara ya kwanza itashuhudia mechi ya soka ya mashindano toka kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilimng’oa madarakani aliyekuwa rais wan chi hiyo hayati Muamar Gaddafi. Mechi hiyo itakuwa ni kati ya wenyeji timu ya Al Nasr yenye maskani yake jijini Benghazi ambao watawakaribisha FAR Rabat ya Morocco katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya timu 16 bora. Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF mwezi uliopita lilitoa ruhusa kwa nchi hiyo kuandaa mechi za kimataifa baada ya hali usalama kurejea. Katika kipindi cha miaka miwili ya machafuko Libya ililazimika kucheza mechi zake za kimataifa katika nchi za jirani Morocco na Tunisia.

No comments:

Post a Comment